Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amezitaka Wizara na Taasisi kuacha mara moja kuajiri Wanunuzi na Wagavi wasiosajiliwa. Makamu wa Rais aliyasema haya wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Makamu wa Rais alisema “Nimefurahishwa sana na utamaduni huu wa kuwa na mkutano wa Wanataaluma ya Ununuzi na Ugavi kila mwaka. Ni utamaduni mzuri kwani unatoa fursa ya kujitathmini, kuelimishana na kuelezana mafanikio na changamoto mbalimbali katika kutekeleza shughuli za ununuzi na ugavi”.